HATUJAMPATA HUYO MDHAMINI ANAONGELELEWA -BEACH BAY FC

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Beach Bay Peter Mole kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi amethibitisha kuwa suala la kupatikana kwa mudhamini ni tetesi ambazo zinaenea mitandaoni na kwa sasa hazina ukweli wowote.

Amezungumza hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa kuna bwenyenye aliyejitokeza kwa nia ya kuifadhili klabu hiyo ya daraja la pili kitaifa kwa masharti klabu hiyo ibadilishe jina kutoka Beach Bay hadi Magarini United.

Mole ambaye kwa sasa ni Kati ya viongozi, wa beach bay amesema kuwa kwa sasa klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kiuchumi jambo ambalo haliwezi kuwafanya kususia ujio wa ufadhili wowote almradi vijana wa Magarini wafaidike.

Mole amesistiza umuhimu wa udhamini akituma wito kwa mtu yeyote anayedhamiria kuifadhili Beach Bay ajitokeze. Amesema katika dirisha hili la uhamisho klabu hiyo inapitia changamoto za kushawishi wachezaji kujiunga na miamba hao wa mjanaheri.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *