Klabu ya Bumbani Stars inalenga kutumia dirisha la sasa la usajili kuimarisha kikosi Chao kuelekea msimu mpya ambao watacbeza katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa baada ya kupanda msimu huu.
Kulingana na Omar Mnyeto ambaye ni Patron wa klabu hiyo ni kuwa wachezaji takriban saba watasajiliwa msimu huu huku klabu hiyo ya LungaLunga tayari ikithibigisha kujaza nafasi Tatu Kati ya hizo saba.
Mnyeto amekanusha tetesi zinazovuma kuwa huenda klabu hiyo imeachana na kocha Mwaduka Bakari aliyeipandisha daraja Bumbani Stars msimu huu. Amesema kwa muda aliondoka kwa matatizo ya ki familia na atarejea katika majukumu yake msimu utakapoanza.

