Nahodha wa zamani wa klabu ya Malindi United Bernard Lusi amethibitisha kuwa ni rasmi ameigura klabu hiyo ya Malindi na sasa amejiunga na klabu ya Equity.
Beki huyo kisiki amethibitisha kuwa akutoelewana na uongozi wa klabu ndio jambo ambalo lilimfanya kuachana na klabu hiyo inayomilikiwa na mwakilishi wadi wa mji wa Malindi Rashid Odhiambo.
Amesema mwsihoni mwa msimu jana klabu hiyo ilifeli kwenye kuwalipa baadhi ya wachezaji jambo ambalo lilianza kuleta mgongano ndani ya klabu na kupelekea baadhi yao ambao ni pamoja na Lusi kuachana na klabu hiyo iliyokuwa inatumia uwanja wa Alaskan kwa mechi zao za nyumbani.
Uongozi wa vilabu vya Malindi Progressive Academy na Malindi United unalenga kufanya kikao wiki ujayo kujadili masuala ya manendeleo ya soka kwenye kambi hizo mbili kuelekea msimu ujao.
Kulingana na kocha wa Malindi Progresive academy Nero Chishenga ambaye ni kati ya viongozi wa ndani sana wa kambi hizo ni kuwa kati ya masuala yanayolengwa kujadiliwa ni kwa mfano ni klabu gani kati ya hizo mbili itashiriki katika ligi gani baada ya msimu uliopita vilabu hivyo kuwa na matokeo duni yaliyopeleka kushuka madaraja.
Nero amethititishia Tama la spoti jioni ya leo kuwa kiungo wao mshambulizi Rafiki Kavoi ameigura kambi hiyo na sio mchezaji tena wa Malindi United. Nero anasema Kavoi aliachilia kipindi cha mashindano ya kitaifa ya KYISA yalofanyika katika kaunti ya Kilifi.