Huenda Kenya ikajipata katika hatari ya kufungiwa tena na fifa kwenye soka la kimataifa kutokana na muingiliano wa serikali na sintofahamu iliyopo katika shirikihso hadi kufikia sasa.
Hiyo ni kulingana na baadhi ya wachanganuzi wa masuala ya sheria na michezo hapa nchini akiwemo wakili wa michezo Japhet Munyendo.
Hii ni baada ya mahakama jana kupiga marufuku shughuli zozote za shirikihso kwenye maandalizi ya uchaguzi mpya pamoja na kufanya vikao vyovyote vya mipangilio ya kuunda fkf mpya.
Amri ya mahakama iliyotoka kwa jaji Janet Mulwa ilisema FKF pamoja na kamati zote imefungiwa kutofanya vikao vyovyote na amri hiyo itasimama hadi tarehe 7 mwezi Octoba kipindi ambacho maafisa wote wa fkf nchini watakuwa tayari washakamilisha vipindi vyao kihalali, kwani vinakamilika katikati ya mwezi September.
Hii ikiwa ina maana kuwa baada ya kipindi hicho hakutakuwa na uongozi wa fkf nchini jambo ambalo baadhi ya wachanganuzi wanasema ni tishio la soka katika taifa hili.
Twaha Mbarak ambaye ni mkereketwa wa masuala ya soka hapa nchini ametuma wito kwa serikali kushauriana na fkf na kamati zake ili kurudisha hali ya sawa nchini.