Mashindano ya olimpiki yanaendelea nchini Ufaransa, na mashindano ya kwanza ya uwanjani yatakayoshirikisha wakenya kwenye riadha ni kuwa kesho kikosi cha wanaume kitashiriki kwenye mashindano ya walking race kilomita 20 kabla mbio za mita 1500, mita 5000, mbio za kupokezana vijiti kuanza rasmi ijumaa wiki hii.
Kwenye soka ni kuwa timu ya taifa ya ufaransa imefuzu kutonga robo fainali ya mashindano hayo. Na hii ni baada ya kuitandika New Zealand kichapo cha mabao 3-0. Ufaransa sasa watachuana na Argetnina kwenye robo fainali.
Marekani nao wamefuzu robo fainali baada ya kuichakaza Guinea kichapo cha mabao 3-0 na sasa kwenye robo fainali watakuwa wanachuana na timu ya taifa ya Morocco. Morocco ilifuzu baada ya kuichapa Iraq bao 3-0.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuzidi kunoga kuanzia kesho ambapo mashindano ya katikati ya viwanja yatakuwa yanaanza rasmi. Kenya inatarajia kuwa na matumaini ya kusajili matokeo mazuri.

