Taifa la Saudi Arabia ndio taifa pekee kwa sasa ambalo limewasilisha ombi la kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la FIFA 2034, itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya timu 48 katika viwanja kumi na tano katika miji mitano, ikiwa ni pamoja na viwanja vinane katika mji mkuu.
Tangazo linajiri siku chache baada ya ufalme huo kuwasilisha ombi lake rasmi kwa FIFA.
Saudi Arabia inapanga kuandaa mashindano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa” katika nchi moja, kulingana na zabuni iliyowasilishwa , na ambayo maelezo yake yalitolewa na Shirika la Habari la Saudi
Watakuwa na viwanja 15 vya hali ya juu, kumi na moja vikiwa vipya, kulingana na shirika hilo.
Riyadh itakuwa nyumbani kwa viwanja vinane, ikiwa ni pamoja na Uwanja mpya wa King Salman, ambao utachukua zaidi ya watazamaji 92,000 na unatazamiwa kuandaa mechi ya ufunguzi na ya mwisho.