MALINDI HIGH IKO TAYARI KWA MASHINDANO YA KITAIFA

Timu ya shule ya upili ya Malindi High inatarajia kuwa na kibarua kigumu kuanzia hapo kesho watakapokuwa wanaanza Kushuka dimbani katika kampeni yao ya kuwania taji la raga za wachezaji saba kila upande kwenye mashindano ya shule za upili huko Kisii.

Kennedy Kirinywa ambaye anaiongoza timu hiyo anasema analenga kuandikisha matokeo bora makala ya mwaka huu ili angalau kuandikisha historia.

Malindi High School ndio inawakilisha mkoa wa Pwani kwenye raga baada ya kufuzu katika mashindano yalofanyika Tana River mwezi July.

Mashindano ya shule za upili hatua ya kitaifa yanaaza rasmi kuanzia kesho katika kaunti ya Kisii michezo kadhaa ikirindima kama Vile Soka, mpira wa wavu, mpira wa Pete, miongoni na michezo mingine

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *