WAZIRI MTEULE MURKOMEN ASHAURIWA

Waziri mteule katika wizara ya Michezo na talanta nchini Kipchumba Murkomen ametakiwa kuhakikisha kuwa anaimarisha shughuli za michezo katika taifa hili.

Kulingana na mwenyekiti wa muungano wa mchezo ya kandanda kaunti ya Mombasa Goshi Juma Ali, kuimarika kwa michezo kutasaidia pakubwa vijana kupata mapato bora na kujiepusha na mambo maovu kwenye jamii.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Juma amesema kuwa hatua hiyo pia itavutia wawekezaji wengi kujitokeza na kufadhili vijana kuboresha talanta zao katika maisha.

Aidha Juma amewanyooshea kidole cha lawama baadhi ya wadau katika mashirika mbalimbali ya michezo humu nchini kwa madai ya kuchangia katika kushuhudiwa kwa mizozo kwenye idara ya michezo kitaifa.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *