MALINDI HIGH YAPANGA KUANDIKISHA HISTORIA KWENYE RAGA

Mwalimu wa michezo katika shule ya upili ya wavulana ya Malindi High kutoka eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi Kenedy Kirinywa anasema anajivunia kuwa wawakilishi wa mkoa wa pwani katika mashindano ya shule za upili mwaka huu kwenye mchezo wa raga za wachezaji saba kila upande.

Kirinywa sasa anasema timu yake inalenga kusajili matokeo mazuri na angalau kuandikisha historia kwenye mashindano hayo yatakayoanza rasmi wiki hii katika kaunti ya Kisii.

Shule ya Malindi High inatarajiwa kuanza safari yake hii leo kuelekea Kisii ambako michezo ya raga itaanza rasmi kuanzia tarehe 2 hadi 8 mwezi Agosti.

Malindi High imewekwa chungu A ambapo kinajumuisha Koyonzo BOYS, Upper Hill ya Nairobi pamoja na wenyeji Kisii School.