TUZO ZA FKF KUVUTIA WENGI MSIMU UJAO

Huenda msimu ujao katika ligi za FKF nchini zikawa na ushindani mkali na viwango bora vya wachezaji kuonekana baada ya tuzo za fkf kufanyika wikendi ilopita ambazo sasa zinatarajiwa kuvutia wachezaji wengi katika siku za usoni.

Ni kauli ambayo imetolewa na Beldine Odemba kocha wa timu ya kinadada ya Kenya Police Bullets aliyeshinda tuzo la kocha bora wa kike msimu ulopita.

Amesema ni fursa ambayo wachezaji na timu nyingi zitajituma zaidi kuwania tuzo kama hizo msimu ujao kutokana na tukio la wachezaji binafsi sasa kuanza kutambuliaka.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na rais wa FKF Nick Mwendwa ambaye ameongeza kuwa maandalizi ya tuzo za wikendi ilopita zinaashiria kuwa mchezo wa soka nchini umeanza kukua na huenda kukazidi kushuhudiwa ushindani mkala kuelekea msimu ujao.