Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka dunia fifa, Sepp Blatter amekiri kwamba maamuzi ya kamati kuu ya fifa kuipa Qatar nafasi ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia ilikuwa makosa.
Kamati hiyo mwaka wa 2010 ilipigia kura Qatar kushinda nafasi hyo kwa kura 14-8 ambapo taifa la marekani lilikuwa linangangania nafasi hiyo.
Amemlaumu Michael Plattini ambaye wakati huo alikuwa rais wa Uefa kwa kupigia kampeni Qatar akisema kwamba walifanya makosa na kwa upande wake Michael Plattini amekataa madai hayo akisema wakati huo demokrasia ya ukweli ilifanyika na Qatar kushinda nafasi hiyo.
Mbali na kwamba mwaka huu walilenga kuleta mashabiki wapya katika kombe la dunia jamii ya kiarabu pamoja na waislamu, hatua hiyo imekuwa ikikashifiwa vikali na wadau wa soka ulaya wanaodai kwamba Qatar iko na sheria kali ambazo huenda zikapunguza mashabiki wengi wenye hamu ya kutazama mashindano hayo.

