SADIO MANE KUKOSA KOMBE LA DUNIA

Sadio Mane wa timu ya taifa ya Senegal, atakosekana katika mashindano ya kombe la dunia mwaka huu kutokana na jeraha alilipata kwenye mechi ambapo klabu yake ya Bayern Munich ilikuwa inavaana na Bremen, jeraha hilo sasa litamlazimu kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki mbili huku mitanange ya kombe la dunia ikitarajiwa kuanza rasmi ndani ya siku 11 zijazo.

Ikumbukwe kwamba Sadio Mane ni kiungo tegemezi kwenye timu yake ya simba wa teranga, ambayo ni timu ya taifa ya Senegal baada ya kuisaidia kufuzu kucheza mashindano hayo baada ya mkwaju wake wa penanty kuisaidia Senegal kuitandika Misri na kujikatia tikiti ya Qatar.

Sadio Mane kwa sasa ndiye mwanasoka bora wa mwaka baada ya kuipeleka timu yake katika fainali za kombe la Afcon, kushinda taji hilo pamoja na kuwa na mafanikio mengine ulaya akichezea klabu ya Liverpool.