KESI ZA KUNAJISIWA WA WATOTO KATI YA UMRI WA MIAKA 16 HADI 18 ZIMERIPOTIWA KWENYE MAHAKAMA YA KILIFI

Hakimu mkaazi mwandamizi katika mahakama ya Kilifi kaunti ya Kilifi Daniel Sitati Sifuma, amesema kesi za kunajisiwa kwa watoto kati ya umri wa miaka 16 hadi 18 zimeripotiwa katika mahakama hiyo kinyume na hapo awali ambapo kesi nyingi zilihusisha watoto wenye umri wa chini ya miaka 10.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku ya kuanza kutoa huduma kwa watoto ambayo huadhimishwa na idara ya mahakama nchini mwezi wa Novemba kila mwaka Sifuma amesema idadi hiyo imeendelea kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma.
Ameitaka idara ya polisi kuwasilisha mahakamani ripoti ya uchunguzi ya kesi husika kwa wakati unaofaa ili kuharakisha kuskizwa kwa kesi zilizoko mahakamani zinazohusiana na visa hivyo ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa washusika iwapo watapatikana na hatia.
Kwa upande wake Elma Sidi Katana afisa wa watoto kutoka shirika la kimataifa la World Vision ameitaka mahakama nchini kuanzisha huduma za kuskiza kesi mashinani ( MOBILE COURTS) hususan sehemu za Bamba kutokana na umbali wa mahakama ili kuhakikisha visa vyote vya dhuluma za watoto vinaripotiwa na kuskizwa kwa wakati ufaao ili waathiriwa waweze kupata haki.