MOHAMED FAKI ATOA WITO KWA SERIKALI KUUNDA JOPO LA KUCHUNGUZA VISA VYA WATU KUULIWA KIHOLELA

Seneta wa kaunti ya Mombasa Mohamed Faki ametoa wito kwa serikali kuu kuunda jopo ambalo litachunguza visa vya watu kuuliwa kiholela na wengine kupotea katika hali tatanishi ili hatua za kisheri dhidi ya wahusika.
Amependekeza uongozi wa jopo hilo liwe mikononi mwa maafisa ambao hawako kwenye idara ya usalama ili waathiriwa wa mauaji hayo wapate haki kwa mujibu wa sheria, akidai huenda waliohusika ikawa watu ambao wanaaminika kuwa maafisa wa polisi.
Amesema ili kumaliza visa hivyo ni lazima serikali iweke Juhudi zaidi ili kufanikisha hilo.