Leo ni siku kuu katika taifa la Saudia Arabia kufuatia tangazo la jana la mfalme wa taifa hilo Salman kusema wananchi wanapasa kusherehekea ushindi wa timu yao ya taifa walipoichana timu ya taifa ya Argentina katika mechi yao ya ufunguzi kwenye mashindano yanayoendelea katika taifa la Qatar.
Saudi Arabia iliitandika Argentina kichapo cha mabao 2-1 na matokeo hayo sasa yanaifanya Saudi Arabia kusimama katika nafasi ya kwanza kwenye kundi C wakiwa na alama tatu.
Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud sasa amefikia rekodi ya nguli wa taifa hilo Thieri Henry, ya kufikisha mabao 51 katika ngazi ya taifa baada ya bao lake la jana alolifunga katika dakika za lala salama kwenye ushindi wao wa kwanza katika mashindano ya kombe la dunia kule Qatar.
Ufaransa walisajili ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Australia na kuenda kileleni mwa kundi D

