Wamiliki wa klabu ya Manchester United walitangaza rasmi hapo jana kwamba wanalenga kuanza mchakato wa kuiuza klabu hiyo baada ya kuimiliki kwa kipindi cha miaka 17 chini ya familia hiyo ya Glazer.
Sambamba na hayo pia walitangaza rasmi kukatisha mkataba wa nyota wa ureno Cristiano Ronaldo kwa maelewano baina ya pande mbili, hii ikimaanisha kwamba Ronaldo baada ya mashindano ya kombe la dunia akiwajibikia timu yake ya taifa ya Ureno atakuwa anafungasha virago vyake na kuanza kutafuta hifadhi sehemu nyingine.
Klabu ya Manchester United imekuwa bila mafanikio katika kipindi cha miaka 9 ilopita tangia mwaka 2013 pale mkufunzi Sir Alex Fergerson alistafu rasmi.
Kwa miaka takriban 10 Man U imekosa kuwa na mafanikio ya primia pamoja na kukaa kipindi cha miaka 5 bila taji lolote licha ya kwamba kipindi hicho, klabu imebadilisha wakufunzi mara kadhaa.
Kwa sasa Cristiano Ronaldo yupo njia panda kuhusu uhamisho wa kwenda Newcastle United au klabu ya Saudi Arabia Al-Nassr kufuatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kuondoka Manchester United
Manchester United imeokoa mishahara ya takriban £15.5m baada ya kufikia makubaliano na Ronaldo kumaliza mkataba wake kabla ya kumalizika majira ya joto.

