Mashindano ya kombe la dunia yanazidi kushangaza wengi na ukistaajabu ya Argentina kupigwa na Saudi Arabia jana meche nyingine ni ya leo ya Ujerumani na Japan ambayo imetamatika kwa Ujerumani kutandikwa kichapo cha mabao 2-1 na Japan mtanange ambao umechezwa katika dimba la Khalifa stadium katikati mwa jiji la doha.
Ikay Gundogan yule wa Manchester City ndiye alikuwa wakwanza kucheka na nyavu na kuwaweka Ujerumani kifua mbele kwenye kipindi cha kwanza kabla ya kuhudi zake kupigwa breki na bao la Ritsu Doan wa Japan kuingia kimyani katika dakika ya 75 ya mchezo.
Mchezaji wa klabu ya Bochum, klabu ya ligi kuu ya ujerumani Bundesliga mwite Takuma Asano katika dakika ya lala salama aliingia kambani na kuzamisha kabisa matumaini ya Ujerumani kuhifadhi alama yeyote katika mechi ya kwanza mwka huu.

