Jaji mkuu wa Mahakama ya Ardhi na Mazingira Dkt. Millicent Odeny amesema maeneo bunge ya Kilifi Kaskazini na Kilifi Kusini kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa yale yanayokumbwa na uskwota kaunti ya Kilifi.
Akizungumza katika kikao na wanahabari mjini Kilifi kaunti ya Kilifi Odeny amesema wakati umefika kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kushughulikia swala hilo na kulitatua kwa mujibu wa sheria.
Odeny amesema kutatuliwa kwa visa hivyo, pia kutasaidia katika kupunguza mrundiko wa kesi za ardhi zilizoko mahakamani.
Jaji huyo amesema kulingana na mahakama endapo kuna swala la majengo Fulani kubomolewa basi zoezi hilo linafaa kutekelezwa mchana na sio usiku na kuhakikisha kuna barua maalum ya kuamurisha kutekelezwa kwa ubomozi huo kutoka mahakamani.
Kwa upande wake gavana wa Kilifi Gideon Maitha Mung’aro amewahimiza wakazi walio na matatizo ya ardhi kuhudhuria vikao vinavyoendelea mjini Kilifi ili kupata fursa ya kukutana na majaji wa ardhi na mazingira watakaowasaidia kukabili tatizo hilo.
MAENEO BUNGE YA KILIFI KASKAZINI NA KILIFI KUSINI MIONGONI MWA YANAYOKUMBWA NA USKWOTA

