MADAI YAIBULIWA VIJANA WA PWANI WANABAGULIWA KWENYE MASUALA YA AJIRA

Mkurugenzi wa shirika la kukabiliana na utumizi wa pombe haramau na dawa za kulevya nchini NACADA Fatuma Rashid amelalamikia ubaguzi dhidi ya vijana wa kanda ya pwani hasa kwenye masuala ya kazi.
Akizungumza kwenye kaunti ya Mombasa Fatuma amesema hali hiyo imekuwa ikichangia kwa idadi kubwa ya vijana kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Fatuma licha ya vijana wengi kusoma na kuwa na stakabadhi hitajika hawajakuwa wakiajiriwa hali ambayo anasema iwapo mikakati thabiti haitaweka kudhibiti hilo huenda wengi wao wakazidi kuwa waraibu wa dawa za kulevya.