Mbunge wa Wundanyi kaunti ya Taita Taveta Danson Mwashako amesema wenyeji wa kaunti hiyo hawajakuwa wakinufaika na shughuli za uchimbaji madini ambazo zinaendelezwa na mwekezaji mmoja wa kibinafsi.
Mwashako anadai mwekezaji huyo amekiuka sheria za uchimbaji madini kwani amekuwa akikwepa kutoa asilimia ya mgao wa fedha kwa wenyeji kutokana na madini hayo.
Aidha, amesema licha ya mwekezaji huyo kuendeleza uchimbaji madini wenyeji pia hawajanufaika na miradi yoyote kutoka kwake au hata ajira.
Amesema ili wawekezaji kwenye kaunti hiyo kuwajibika ipasavyo ni lazima viongozi wa Taita Taveta washirikiane vyema katika kufanikisha hilo.
DANSON MWASHAKO ADAI WENYEJI WA WUNDANYI HAWAJAKUWA WAKINUFAIKA NA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI

