Wahudumu wa afya wa nyanjani kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa Serikali ya kaunti ya Kilifi na idara ya afya kwa jumla kuwatambua katika utendakazi wao wanaofanyia jamii.
Wakiongozwa na Michael Ruwa almaarufu Kadzaya Wanadai kutotambuliwa na serikali ya kaunti ya Kilifi pamoja na wahudumu wa afya katika hospitali za kaunti ya Kilifi hususan hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi hali wambayo wameitaja kuwa changamoto kuu katika kutekeleza vyema majukumu yao nyanjani.
Amewataka wahudumu wa afya katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi kuwatambua na kutilia maanani kazi wanazo zitekeleza nyanjani.
Wakati uohuo Ruwa ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kupitia gavana Mung’aro kuwatambua na kuwawezesha kifedha ili waweza kuimarisha utendakazi wao.
WAHUDUMU WA AFYA WA NYANJANI KAUNTI YA KILIFI WALALAMIKA

