GAVANA DHADHO GODHANA ATAKIWA KUWASILISHA MAJINA YA MAWAZIRI WATEULE

Mwakilishi wa wadi ya Garsen ya Kati kaunti ya Tana River Masha Boru amemtaka gavana wa kaunti hiyo Dhadho Godhana kuwasilisha orodha mpya ya majina ya mawaziri wateule baada ya mawaziri watatu waliopendekezwa na gavana huyo kukosa kuidhinishwa na bunge la kaunti ya Tana River.
Boru ambaye aliwahi kuhudumu kama kiongozi wa wengi kwenye bunge la kaunti ya Tana River amesema ni lazima Gavana huyo kuwasilisha orodha yote ya mawaziri wateule bungeni kwa mujibuwa wa sheria.
Masha Boru amewataka watumishi wa umma kuwahudumia wenyeji na sio kujihusisha na siasa kwani ni kinyume cha sheria.