Mkufunzi mkuu wa klabu ya Birmingham City Wayne Rooney amefutwa kazi rasmi na klabu hiyo kutokana na msururu wa matokeo duni katika ligi ya daraja la Championship msimu huu.
Rooney amesajili ushindi mara mbili pekee katika mechi 15 alizowaongoza Birmingham City na kuipeleka klabu hiyo kutoka nafasi ya 6 alipoajiriwa hadi sasa nafasi ya 20 katika ligi hiyo.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Everton, Machester United na timu ya taifa ya Uingereza mwenye umri wa miaka 38 amekuwa Birmingham kwa kipindi cha miezi minne pekee.
Muda mfupi baaada yakufutwa Rooney ametoa taarifa za shurani kwa wajiri wake kwa kumpa nafasi ya kuongoza klabu hiyo kwa kipindi cha wiki 13.Amedokeza kuwa hakuwa na muda wa kutosha kusuka kikosi chenye ushindani kama mkufunzi jambo ambalo limesababisha matokeo duni.
Pia ameonyesha kutambua kuwa soka ni biashara ambayo inalipwa na kupewa heshima na mpunga unaotokana na matokeomazuri uwanjani. Hata hivyo amewatakia kila la heri Birmingham City anapoenda kupumzika masaibu

