HATUPOTEZI MECHI TENA – BEACH BAY

Klabu ya Beach ina imani itazidi kuandikisha matokeo mazuri msimu huu baada ya kuzoa alama nne katika mechi mbili wikendi hii, tatu dhidi ya Kamtonga na moja dhidi ya Jr FC.

Kulingana na Clara Kadzo ambaye ni afisa wa klabu hiyo ni kuwa uchovu ndio sababu iliyowafanya kutovuna alama zote wikendi katika mechi hizo mbili walizocheza katika kaunti ya taifa taveta.

”Tulienda Taita kushinda sisi, hayo ndiyo yalikuwa malengo yetu kwenye mechi zote mbili. Lakini kutokana na uchovu tulipiga sare katika mechi ya pili na ilikuwa dhidi ya Junior FC ya 2-2 lakini awali tulikuwa tumewapiga Kamtonga FC 2-1.” Alisema Clara

Clara anaimani klabu yake ikaendeleza msururu wa matokeo ya kuridhisha huku ikiwa kwa sasa inasimama katika nafasi ya saba na alama 10 katika ligi ya daraja la pili.

”Kuanzia sasa sidhani kama Beach Bay tutapoteza mechi yoyote. Vijana wameimarika sana” Aliongeza Clara