Mchezaji wa timu ya taifa ya Harambe Starlets Essie Akida anapania kuanzisha mashindano ya soka mwishoni mwa mwezi huu.
Malkia huyo anayechezea klabu ya AC PAOK Thessaloniki yenye makazi yake ugiriki analenga kuandaa mashindano hayo aliyoyapa jina la Essie Akida Football Tournament mashindano ambayo yatafanyika katika uwanja wa Mkoroshoni mjini kilifi kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Akida ambaye ametupia chapisho kwenye ukurasa wake wa facebook ni kuwa anaandaa mashindano hayo kama njia moja ya kurudisha mkono kwa jamii.
Akida ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Moving The Goal post yenye makazi yake Kilifi ambayo kwa sasa inaongozwa na mkufunzi Fathime Tibu.

