MCHEZO WA TONG IL MOO- DOO IMEPIGA HATUA NCHINI – MWAKIO

Rais wa mchezo wa Tong IL Moo – Doo nchini Clarence Mwakio amesema kwamba mchezo huo umeanza kupiga hatua katika umaarufu wako katika taifa hili la Kenya.

Ametoa wito kwa vijana wengi kujisajili kwa mchezo huo huku akithibitisha kuwa tayari Tong ill Moo – Doo imefika katika kaunti  14 kufikia sasa huku akiwa anapania kuimarisha zaidi umaarufu wa mchezo huo na kufikia kaunti zote 47.

”Kwa sasa mchezo huu umepiga hatua hapa nchini Kenya. Tuko katika kaunti 14 kati ya 47. Tunapania kuufikisha mchezo huu kwa kaunti zote mwishoni mwa mwaka 2024. Pia tunalenga kuusambaza hata zaidi katika bara zima la Afrika ambapo kuna uhitaji mkubwa wa talanta za mchezo huu.” Alisema Mwakio

Mwakio ameongeza kuwa kuna uhitaji mkubwa wa talanta za mchezo huo kwa sasa ulimwenguni.

Amesema kwamba mbali na mafunzo ya Tong Ill Moo – Doo kama silaha  ya kujilinda kwa mtu binafsi pia yanaweza kutumika kama ajira ikizingatiwa kuwa mataifa mengi barani afrika na ulimwengu kwa ujumla yanauhitaji wa  wachezaji wenye talanta za mchezo huo.