Katibu katika Wizari ya Michezo Peter Tum hapa nchini Kenya amefichua kwamba Wizara hiyo ilikuwa imetumia Sh.532 milioni kwa Mpango wa Talanta Hela katika kipindi cha mwaka mmoja huku akishikilia kuwa programu hiyo ilikuwa hatua kubwa ya kuleta mabadiliko katika michezo ya Kenya.
Tum alisema hayo alipofika mbele ya Kamati ya Michezo ya Bunge la Kitaifa kutoa mwanga kuhusu programu hiyo iliyoanzishwa mwaka jana,na inayolenga kuibua, kuajiri na kukuza, soko na uchumaji kupitia vipaji.
Tum aliongeza kuwa mpango huo unaipa Kenya nafasi ya kutambua vipaji vipya ambavyo vinaweza kusaidia pakubwa kusaidia taifa hili kukua kama taifa la michezo na sanaa.

