Serikali ya Kenya imefikia makubaliano ya ushirika na taifa la Morocco kuhusu masula ya ya ukuzaji wa talanta za wachezaji wenye umri mchanga baina ya mataifa yote mawili.
Hii ni baada ya jana waziri wa michezo hapa nchini Ababu Namwamba kusaini mkataba huo na waziri wa michezo na sanaa wa Morrocco Chakib Benmoussa.
Waziri Namwamba ameeleza umuhimu wa ushirikiano huo akihoji kuwa Kenya iko na mengi ya kujifunza kutoka Morocco ambao katika miaka ya hivi punde wamekuwa na mafanikio makubwa kwenye soka hasa katika mashindano ya kombe la dunia walifika katika semi fainali mwaka 2022.

