PEP GUARDIOLA KUKOSA MECHI MBILI ZA EPL

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anatarajiwa kukosa mechi mbili zijazo baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye mgongo wake hii leo.

Pep Guardiola ambaye amekuwa akikabiliwa na maumivu ya mgongo kwa muda ameachiliwa na klabu yake kufanyiwa upasuaji.

Kulingana na taarifa ambayo imeachiliwa na Manchster City leo ni kuwa Guardiola atakosa mechi ya Sheffield United pamoja na ile ya Fulham FC tarehe 2 mwezi September.

Manchester City katika mechi mbili za mwanzo msimu huu wamesajili ushindi zote (1-0 dhidi ya Burnley na 1-0 dhidi ya Newcastle United) na sasa wanasimama katika nafasi ya pili ligini na alama 6.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *