Wito umetolewa kwa timu za soka katika kaunti ya kwale kushirikiana na shirikisho la soka katika tawi la gatuzi hilo kusajili wa wachezaji kwa ajili ya mashindano ya chapa dimba ambayo yatakuwa yanachezwa katika ngazi ya kaunti.
Kulingana na taarifa iliyowasilishwa kwa vilabu na mkurugenzi mkuu wa FKF Kwale bwana Shaban Mwero ni kuwa vilabu hivyo vinafaa kufanya usajili wa wachezaji wa kati ya umri wa miaka 16-19 huku usajili huo ukitarajiwa kutamatika tarehe 8 mwezi September mwaka huu.
Baada ya kikao cha jana, shirikisho la FKF katika ngazi ya kaunti ya Kwale imethibitika kuwa mshindi wa mashindano ya Chapa Dimba makala ya mwaka huu atakuwa anajishindia 70,000 pesa taslimu za Kenya.