NIPENI MUDA NIUNDE KIKOSI – ENGIN FIRAT

Mkufunzi mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Harambee Stars Engin Firat anasema wakenya wanafaa kuwa na subra naye ili atengeneze kikosi ambacho kitakuwa na uwezo wa kuleta ushindanio katika mechi za kimataifa.

Mkufunzi huyo wakati akizungumza na vyombo vya habari amesema hataahidi wakenya matokeo mazuri mara moja kwani sasa ako na kazi ya kusuka kikosi chake wanapojitayarisha kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Iran tarehe 28 mwezi huu.

Firat amehoji kwamba kwa sasa taifa la Kenya liko na safari ndefu kuhakikisha michezo inaimarika ikizingatiwa kwamba hakuna viwanja vya hadhi ya fifa hasa katika kaunti nje ya jiji la Nairobi ambako kunaviwanja viwili ambavyo bado vinahitaji kukarabatiwa kufikia hadi hiyo.