BARCA YASELELEA KILELENI MWA LALIGA

Klabu ya Barcelona sasa imerefusha pengo lao na nafasi ya pili katika ligi ya laliga hadi alama 12 baada ya kuichapa real Madrid mabao 2-1 katika mchezo wa el classic uliochezwa jana katika dimba la Camp Nou.

Madrid walipata bao la kwanza kupitia beki wa Barcelona Ronald Araujo kujifunga lakini Sergio Roberto akasawazisha bao hilo katika kipindi cha kwanza na hatimaye Frank Kessie nyota wa kimataifa wa Ivory Coast akafungia Barca ya Xavi Hernandez bao la ushindi katika dakika za lala salama.

Kwa sasa vijana Barcelona wapo makini kusajili ushindi wao wa kwanza wa laliga chini ya mkufunzi Xavi Hernandes baada ya kukaa kipindi kirefu bila kushinda taji hilo.