MECHI YA YANGA KUCHEZWA KESHO KISA MASHINDANO YA UFUKWE

Mechi ya daraja la pili kitaifa ya Samburu Lions dhidi ya Yanga itachezwa kesho katika dimba la Alaskan mjini Malindi.

Mechi hiyo ilifaa kuchezwa wikendi ilopita lakini ikalazimishwa kuahirishwa kutokana na Yanga fc waliokuwa wanashiriki katika mashuindano ya kitaifa ya Olimpiki za Ufukweni mjini Malindi katika kaunti ya Kilifi ambako Yanga inayoongozwa na mkufunzi Collins Omol kumaliza katika nafasi ya tatu.

Matokeo ya mechi nyingine za daraja la pili ni kwamba Furunzi walisajili ushindi wa 4-3 dhidi ya vijana wa Lamu Deep Sea fc.

Kantonga ya taita taveta ilisajili ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ashton Rangers na hatimaye Sparki Youth katika uwanja wa ugenini wamesajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ziwani Youth.