Nick Mwendwa amerejea kwenye wadhifa wake wa urais wa shirikisho la soka la FKF baada ya kujiuzulu miezi tisa iliyopita kutokana na waziri wa michezo balozi Amina Mohamed kuvunjilia mbali shirikisho hilo pamoja na Mwendwa kustakiwa na makosa ya ubadhirifu wa fedha za michezo pamoja na matumizi mabaya ya kiofisi.
Katika waraka alioandika Mwendwa kwa Rais wa soka duniani FIFA Gianni Infantino, amemwambia kiongozi huyo kuwa amerejea wadhifa wake baada ya idara ya mashtaka ya umma kuondoa mashtaka ya ufisadi dhidi yake.
Katika waraka huo mwendwa ameongeza kuwa sasa kama rais wa shirikisho hilo wanalenga kuanza mchakato wa kuanzisha harakati za kuliondoa taifa la Kenya kwenye marufuku ya kutoshiriki mechi za kimataifa, marufuku iliyoadhibiwa kwa taifa hili baada ya serikali kuingilia masuala ya shirikisho la fkf.
Awali jaji wa mahakama ya juu aliyekuwa anasikiliza kesi iliyokuwa inamshtaki Nick Mwendwa, Esther Maina alikuwa ameweka tarehe 21 mwezi huu kama siku ya kusikilizwa kwa mashtaka mapya dhidi ya mwendwa ili kubaini iwapo Rais huyo wa soka alikuwa ameshtakiwa kulingana na sheria.
Hayo ya kijiri, wiki hii mbunge mteule wa dagoreti kaskazini Betrace Elachi alisema kuwa, analenga kuwasilisha mjadala katika bunge la 13 ili kuona kwamba soka la Kenya linakombolewa kutokana na masaibu yanayosibu mchezo huo hapa nchini.

