Visa vya utapiamlo miongoni mwa watoto vimetajwa kuongezeka kaunti ya Tana River kufuatia hali ya ukame.
Idara ya afya kaunti hiyo ya Tana River imesema watoto waliochini na umri wa miaka 5 wameathirika na utapiamlo kwa asilimia 14.
Kulingana na Dkt. Oscar Endekwa ambaye ni mkurugenzi wa matibabu idara ya afya kaunti ya Tana river amesema idara hiyo ya afya imesema kukauka kwa mabwawa ya maji kumechangia ukosefu wa lishe bora kwani wakaazi wengi wameshindwa kupata chakula kutokana na ukosefu mkubwa wa maji.
WATOTO WALIOKO CHINI YA UMRI WA MIAKA 5 KAUNTI YA TANA RIVER WANAUGUA UTAPIAMLO

