Gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro amesema kuwa malimbikizi ya madeni ambayo yapo katika serikali ya kaunti ya Kilifi yatalipwa pindi uchunguzi wa kina kuhusu madeni hayo utakapokamilika.
Kauli ya gavana Mung’aro imechochewa na taarifa kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 1.4 huku gavana Mung’aro akibainisha kuwa makadirio ya bajeti ya kaunti mwaka 2022 – 2023 hayatatizwa na madeni hayo.
Aidha Mung’aro ameweka wazi kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi italipia miradi iliyokamilika na wala sio miradi hewa hivyo wale waliopata zabuni za kutekeleza miradi isiojulikana ni wazi kuwa hawatawezwa kulipwa.
GAVANA GIDEON MUNG’ARO ASEMA MALIMBIKIZI YA DENI KAUNTI YA KILIFI YATALIPWA

