NGARAMBE ZA SHULE YA UPILI KUANZA RASMI

Michezo ya Shule Za Sekondari kata ndogo ya Malindi imeratibiwa Kupigwa Hapo kesho Tarehe Ishirini na Nane, na Siku ya Alhamisi Tarehe ishirini na Tisa katika Uwanja Wa Shule Ya Malindi High, vyuo Hivyo Vikisaka Nafasi ya Kufuzu kwenye Hatua ya Kaunti.

Shule ya Upili ya Muyeye, Kibokoni, Barani na Sabaki, Zimepangwa kwenye Kundi A Ya soka la wanaume, kundi B likiwakutanisha Kijiwetanga Wenyeji Malindi high na Majivuni, Huku makundi hayo Pia Yakitumika kwenye soka La Kina Dada.

Kwenye Mpira wa Wavu Sabaki , Malindi High, majivuni muyeye na Kijiwetanga watamenyana Kwa Upande wa Wanaume, Huku Vipusa wa Shule ya Upili ya Barani, kibokoni, majivuni na Kijiwetanga wakipimana maji kwenye Mchezo Huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *