Klabu ya Liverpool Ndiyo Inayoongoza Na Idadi ya viatu vya Dhahabu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa na ujumla ya idadi ya Wachezaji Nane hii ni baada ya Mo Salah, Kushinda Tuzo Hilo baada ya Msimu huu Wa Mwaka wa Elfu Mbili ishirini na Nne ishirini na Tano, Kutamatika Siku ya Jumapili.
Arsenal wanashikilia nafasi ya pili na idadi ya wafungaji bora sita kwa Msimu, Manchester United ya Tatu na wachezaji wa Tano sawia Na washindi wa Kombe la Europa Tottenham, Chelsea na Manchester wakifunga nne bora na Ujumla ya Wachezaji wanne.
Mo salah alipiga magoli ishirini na Tisa Msimu Huu Kunyakua Tuzon Hilo, Mswidi Alexander Isak anayekipiga na Newcastle akifuata na Magoli sita Nyuma, mshambuliaji wa Manchester Haaland akimaliza tatu Bora na Magoli ishirini na mawili.

