RONALDO, FIFA CLUB WORD CUP. KUNANI?

Cristiano Ronaldo amechapisha ujumbe wa kutatanisha kuhusu mustakabali wake, hii ni  baada ya Rais wa FIFA Gianni Infantino kusema kuwa mazungumzo yanaendelea, kumhusu mshambuliaji huyo kushiriki katika Kombe la Dunia la vilabu.

Kwa sasa Ronaldo anachezea klabu ya Al Nassr inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia, lakini klabu hiyo haikufuzu kwa toleo jipya la mashindano hayo ya timu thelathini na mbili  yatakayofanyika majira ya kiangazi huko Marekani.

Mkataba wa Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka arubaini  unatamatika msimu huu wa joto, na itahitajika aachiliwe mapema kutoka kwa mkataba huo, ili ajiunge na klabu itakayoshiriki Kombe la Dunia la vilabu ambalo litaanza tarehe kumi na nne mwezi Ujao.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *