NERO ANAAMINI MSIMU UJAO YUPO DARAJA LA KWANZA KITAIFA

Mkufunzi wa Furunzi FC Nero Chishenga ameeleza imani kwamba atasajili ushindi wa pili katika ligi ya daraja la pili kitaifa vijana wake watakapokuwa wanashuka dimbani kesho dhidi ya klabu ya kishada katika uwanja wa Alaskan, uwanja uliopo mjini malindi kaunti ya Kilifi.

Akizungumza na tama la spoti jioni ya leo katika uwanja wa mazoezi ulioko furunzi, mkufunzi Nero amesema kwamba vijana wake wamezidi kuimarika na kurekebisha makosa ambayo yaliwaponza katika mechi ya kwanza walipofungwa na omax kichapo cha bao 5-2 mjini Mombasa

Mkufunzi Nero pia ametoa hakikisho kwa mashabiki wa klabu yake kwamba msimu ujao watapanda daraja hadi Daraja la kwanza kitaifa kuungana na Malindi Progressive pamoja na Young Bulls ambazo ndio klabu pekee kutoka malindi zinazoshiriki ligi ya daraja la kwanza.

Amesema kwamba vijana wake wanamotisha wa kufanya vyema katika ligi jambo ambalo linampa mkufunzi huyo matumaini makubwa ya mafanikio kwenye msimu wa 2022/2023.