Huduma za afya kwenye kaunti ya Mombasa zinatarajiwa kuimarika hata Zaidi hususan maeneo ya mashinani.
Hii ni baada ya jopo kazi linalohusika na masuala ya afya kaunti ya Mombasa kutoa ripoti ya mapendekezo jinsi itakavyoboresha sekta hiyo.
Akizungumza alipokuwa anatoa ripoti hiyo, mwenyekiti wa jopo hilo Chibanzi Mwachonda amesema wametenga baadhi ya Hospitali zitakazotoa huduma maalum za afya kwa wakaazi wa Mashinani.
Wamependekeza Zahanati ya Tudor kuwa ya huduma za matibabu ya watoto na uzazi na hospitali ya Likoni kuwa ya masuala ya upasuaji, Hospitali ya Mvita masuala ya Macho nayo hospitali Kuu ya Ukanda wa Pwani tawi la Utange iwe inatoa huduma za magonjwa ya kuambukiza na pia kuwa kituo cha utafiti wa masuala ya matibabu.
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amepigia upatu mapendekezo kutoka kwa jopo hilo na kusema ni hatua nzuri ya kuimarisha sekta ya afya kaunti ya Mombasa.
Vilevile amesema ameweka mikakati mwafaka kuhakikisha anaziba mianya yote inayotumiwa katika ufajaji wa pesa katika sekta ya afya.
HUDUMA ZA AFYA KAUNTI YA MOMABASA HUENDA ZIKAIMARIKA

