MWALIMU MKUU WA SHULE YA UPILI YA MUYEYE MJINI MALINDI ALALAMIKIA ONGEZEKO LA IDADI YA WANAFUNZI WANAOTUMIA MIHADARATI

Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Muyeye mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Francis Kazungu amelalamikia ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaotumia dawa za kulevya shuleni humo.
Kulingana na mwalimu huyo, wanafunzi wengi wamekuwa wakiingiza dawa hizo za kulevya shuleni humo kutokana na kile ambacho anasema kuchangiwa na ukosefu wa uzio mzuri.
Akizungumza katika kikao cha kutoa mapendekezo ya miradi wanayotaka kufanyiwa na hazina ya NG-CDF katika eneo bunge la Malindi, mwalimu huyo ameitaka bodi ya hazina hiyo kuidhinisha ujenzi wa ua katika shule hiyo, pamoja na ile ya upili ya wavulana ya Malindi.
Wakati uohuo Kazungu ambaye pia ni mwenyekiti wa walimu wakuu katika eneo la MAlindi kaunti ya Kilifi, amesema visa vingi vya utovu wa nidhamu katika shule ya upili ya wavulana ya Malindi, vimechangiwa na ukosefu wa uzio mzuri katika shule hiyo.