GAVANA WA KAUNTI YA KWALE AWAONYA MAKATIBU KATIKA KAUNTI HIYO

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amewaonya makatibu katika kaunti hiyo kutokana na kile anachosema baadhi yao wamechukua zabuni ambazo zinastahili kupewa wakaazi ili waweze kujiinua kimaendeleo.
Achani aliyekuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Kwale amewataka mawaziri wa kaunti hiyo kuhakikisha hakuna ubaguzi wowote unaofanyika katika utoaji wa zabuni akisema ni jukumu la serikali ya kaunti kutoa nafasi za ajira kwa vijana.
Aidha, Achania ameahidi kufanya uchunguzi wa zabuni zinazotolewa pamoja na wenye kampuni na kuwataka makatibu kutoa nafasi kwa wakaazi wa kaunti ya Kwale ili nao pia wafaidike kutokana na zabuni zinazotolewa na serikali ya kaunti hiyo.