JUMLA YA WANAFUNZI 109 KATIKA SHULE ZA UPILI KAUNTI YA KILIFI WANUFAIKA NA MASOMO YA DINI

Jumla ya wanafunzi 109 katika shule za upili kaunti ya Kilifi wamenufaika na masomo ya dini, katika kongamano la wanafunzi wa dini ya kikristo la Rafiki Wa Yesu Youth Camp, lililofanyika jana katika shule ya upili ya wavulana ya Gede, na kufadhiliwa na kituo cha habari cha Lulu fm.
Kulingana na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo kaunti ya Kilifi, Joshua Edwards licha ya idadi ndogo ya wanafunzi kujitokeza katika kongamono hilo, wana matumaini ya wanafunzi hao kuimarika zaidi kiimani.
Akizungumza na lulu Fm baada ya kukamilika kwa kongamono hilo, Joshua ametoa wito kwa wazazi kaunti ya Kilifi, kuwapa watoto wao fursa ya kuhudhuria kongamano hilo ili kunufaika kutokana na mafunzo mengi ya kiunga ambayo yatawasaidia katika maisha.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo wakiongozwa na Faith Zawadi, Salama Saumu pamoja na Adam Jimba, wameelezea kunufaika na masuala mengi ya kuwaimarisha kiimani na kutoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria kongomano hilo ili kujengeka kiimani wanapokuwa shuleni.