Mwaniaji wa kiti cha urais wa Shirikisho la Soka la Kenya Tom Alila ametoa wito kwa Waziri mpya wa Michezo Kipchumba Murkomen kutimiza ahadi yake ya kuboresha mashirikisho ya michezo nchini.
Hayo yanajiri baada ya Murkomen ambaye alikuwa Seneta wa Elgeyo Marakwet kuapishwa leo asubuhi, akimrithi Ababu Namwamba aliyetimuliwa mwezi uliopita.
Alila anahisi mengi yanaweza kuafikiwa ikiwa Murkomen atafanya kama alivyoahidi wakati wa kuhakikiwa kwake na Bunge la Kitaifa. Murkomen katika mahojiano na wabunge alisema kuwa analenga kuhakikisha chaguzi za mashirikihso kufanyika akijadili kuwa mashirikihso mengi yamefeli wakenya hasa FKF ya Nick Mwendwa.
Wakati wa kikao cha mchujo, Murkomen aliapa kukabiliana na viongozi ambao wamekwama katika mashirikisho zaidi ya muda wao kwa mujibu wa sheria.

