Kipchumba Murkomen amekula kiapo hii leo na kuchukua majukumu rasmi kama waziri wa michezo hapa nchini kwenye nafasi ilokuwa inashikiliwa na Ababu Namwamba.
Hii ni baada ya kusailiwa bungeni na baadaye kupitishwa kwa kiapo hicho katika Ikulu ya Nairobi mbele ya Rais wa Kenya William Ruto.
Kati ya mageuzi ya kwanza ambayo Kipchumba aliweka wazi iwapo angepata u waziri ni kuhakikisha uchaguzi wa mashirikisho yote unafanyika mwaka huu hasa katika shirikisho la FKF.
Kabla ya kuteuliwa na Ruto Murkomen alihudumu nchini kama waziri wa barabara na uchukuzi kabla ya kufutwa katika wizara hiyo baada ya shinikizo la wakenya wengi walioandamana ili baraza la mawaziri livunjiliwe mbali.
Hata hivyo Murkomen alirudishwa kwenye baraza na sasa wizara ya talanta na michezo ya vijana. Ameahidi kuwatimua maafisa wa FKF katika shirikisho hilo pamoja na viongozi wengine wa mashirikihso ambao wamekaa sana bila kufanya uchaguzi.

