Klabu ya Young Bulls inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa inaripotiwa kuwa iko kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu ya Ss Asad Ali Mwachaunga.
Mwachaunga aliachana klabu ya SS Assad kabla ya kutamatika kwa msimu uliopita baada ya kukosa kuelewana baadhi ya viongozi na wachezaji wengine wa kikosi ndiposa akajiuzulu.
Pale Young Bulls iwapo mazungumzo yataenda sawa huenda akachukua majukumu ya ukocha kutoka kwa Coach Shaffie ambaye inaripotiwa kuwa aliondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Hii ni kati ya hatua za kuijenga upya klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa mwaka 2024/2025 Bulls ya Malindi ikiwa ndio klabu pekee inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza kitaifa.

