Mechi ya semi fainali ya Dola Super Cup kaunti ya Kilifi raundi ya kwanza ilokuwa inakutanisha timu ya Magarini dhidi ya Kilifi Kusini imetamatika muda mchache uliopita katika uwanja wa GFC Gongoni eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi na imeisha kwa wageni Kilifi Kusini wakisajili ushindi wa bao 1-0.
Suleiman Bareho ambaye ni kocha wa Magarini amesema ameona mchezo mzuri kutoka kwa wapinzani wake na kuwapongeza baada ya kupigwa bao katika kipindi cha pili. Hata hivyo anasema mechio ya marudiano wanakwenda kulipiza kisasa.
Kwa upande wake Mohamed Mangi kocha wa kilifi Kusini anasema analenga kusajili ushindi tena katika mechi ya marudianoitakayopigwa katika uwanja wa Kanamai Kilifi Kusini wakiwa nyumbani kwao.
Mfungaji wa bao hilo la ushindi Dennis Charo ambaye pia amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya leo amekiri kuwa Magarini wameonyesha mchezo mzuri hata kama wamewafunga ugenini.

