MOTSEPE ACHAGULIWA TENA

Patrice Motsepe amechaguliwa tena kama rais wa shirikihso la soka barani Afrika CAF bila kupingwa kwenye zoezi la uchaguzi lililofanyika katika jiji la Cairo, Misri.

Muhula huu ni wa pili kwa Motsepe mwenye umri wa miaka 63 ambaye alitangaza mwaka jana kuwa analenga kusimama tena kutetea kiti hicho mwaka huu.

Mmiliki huyo wa klabu ya ligi kuu ya Afrika Kusini Mamelodi Sundowns ametangazwa jana katika hafla ya uchaguzi ambayo pia ilihudhuriwa na rais wa FIFA Gianni Infantino.

Motsepe alichaguliwa mwaka 2021 katika muhula wake wa kwanza wa miaka minne kuchukua nafasi ya Ahmad Ahmad wa Madagascar ambaye alikuwa amepigwa marufuku na FIFA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *