WITO WA VIWANJA WATOLEWA KILIFI

Mwenyekiti wa FKF Kaunti ya Kilifi Dickson Angore amemhimiza Gavana Mung’aro, na idara yote ya Michezo Kilifi Kaunti Kuharakisha Ujenzi wa kiwanja cha Water Mjini Kilifi, ili kuimarisha vipaji vya soka katika Kaunti hii ya Kilifi.

Kulingana na Angore kiwanja Hicho ambacho baada ya Kukamilika, Kitakua Kiwanja cha Kipekee ndani ya Kilifi Kaunti kimechukua muda mrefu kukamilika, hivyo basi kutatiza Mipangilio ya soka Katika Kaunti Hio.

Akiongezea amedokeza kwamba Licha Ya Serikali ya Kilifi Kuahidi Ujenzi Huo kwa uHaraka, Kiwanja Hicho kimesalia kua ndoto tu.

Aidha Angore ameendelea kwa Kusema kwamba Kupitia miundo msingi kama Hiyo, tutaweza kuuza Soka la Kaunti huko nje na Kuvutia washikadau Mbalimbali, Huku mkufunzi wa Kakoneni All stars  Baha Edward aliyeandamana na Angore, akimalizia kwa kusema ya kwamba ni aibu kwa Kaunti ya Kilifi kukosa kiwanja Tajika, zaidi ya Miaka kumi sasa Baada ya Ugatuzi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *